Kesi ya ubakaji yamtupa jela miaka 4 Dani Alves
Sisti Herman
February 22, 2024
Share :
Aliyekuwa beki wa Barcelona na timu ya Taifa Brazil Dani Alves amepatikana na hatia ya kumdhalilisha kingono mwanamke katika klabu ya usiku ya Barcelona mwaka 2022 na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela.
Mahakama nchini Uhispania imempata nyota huyo na hatia ya kumbaka mwanamke katika klabu ya usiku Desemba 2002. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 amehukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi sita jela na kuamriwa kumlipa mwathiriwa kiasi cha Euro 150,000.
Alves alikamatwa Januari 2023 na amezuiliwa tangu wakati huo baada ya maombi ya dhamana kukataliwa. Waendesha mashtaka walikuwa wakitafuta kifungo cha miaka tisa jela kwa mwanasoka huyo wa zamani.
Taarifa ilisema: "Hukumu hiyo inazingatia kwamba imethibitishwa kuwa mwathiriwa hakukubali, na kwamba kuna ushahidi, pamoja na ushuhuda wa mlalamikaji, kuzingatia ubakaji uliothibitishwa."