Kesi ya uhaini ya Lissu yaahirishwa hadi Julai 15
Sisti Herman
July 1, 2025
Share :
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Julai 15, 2025 ikiwa bado inasubiri hatua atayoichukua Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) akimaliza kupitia faili, ambalo imeelezwa na Mawakili wa Jamhuri kuwa bado lipo mezani kwake
Akizungumza kabla ya maamuzi hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu aliiomba Mahakama iwaamuru Mawakili wa Jamhuri kueleza hatua ya uchunguzi ilipofikia, kwa kuwa hadi kufikia Wiki inayofuata atakuwa amekaa gerezani kwa Siku 90