Kevin Campbell afariki dunia, Arsenal na Everton wamlilia
Eric Buyanza
June 15, 2024
Share :
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal na Everton Kevin Campbell amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 54 baada ya kuugua ugonjwa ambao haujawekwa wazi.
Campbell alilazwa hospitali mapema mwezi huu baada ya kuugua ghafla.
Nyota huyo wa zamani kunako Premier League alipitia akademi ya Arsenal, akajiunga nao akiwa na umri wa miaka 18.
Akiwa na Washika bunduki hao wa jiji la London, alicheza mechi 210 na kufunga mabao 55 katika kipindi cha miaka 10.