pmbet

Khamenei azikwa katikati ya mashambulizi mapya Iran

Eric Buyanza

July 10, 2026
Share :

Hatimaye mazishi ya Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, yamefanyika katika mji wa Mashhad, huku yakifunikwa na mashambulizi mapya kati ya Marekani na Iran.

 

Kulingana na vyombo vya habari vya Iran jana Alhamisi, mazishi yake yalifanyika bila kuhudhuriwa na umma na yalifanyika katika Madhabahu ya Imam Reza, huko Mashhad alikozaliwa baada ya takriban wiki nzima ya maombolezo.

 

Mazishi hayo pia yalifanyika chini ya ulinzi mkali. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, ndege ya kivita iliandamana na ndege iliyobeba jeneza la Khamenei kuelekea Mashhad, huku mamlaka zikifunga anga la mji huo kwa sababu za kiusalama. Huduma za reli kati ya Tehran na Mashhad pia zilisitishwa kwa muda baada ya sehemu ya njia hiyo kushambuliwa.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet