pmbet

Kiasi cha wahamiaji 180 wafariki baharini ndani ya siku 10

Eric Buyanza

April 8, 2026
Share :

Shirika la IOM lasema watu wasiopunguwa 1,000 wamepoteza maisha baharini tangu mwanzoni mwa mwaka 2026.

 

Umoja wa Mataifa umearifu kwamba zaidi ya watu 180 wanakihofiwa wamefariki au kutoweka ndani ya siku 10 zilizopita kufuatia meli kuzama kwenye bahari ya Mediterania.
 

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kimataifa la wahamiaji la Umoja huo IOM vifo vya takriban watu 1,000 vimeripotiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na kuufanya kuwa mwaka ulioshuhudia vifo vingi zaidi tangu mwaka 2014.
 

Shirika hilo limeyataja matukio mbali mbali ya kuzama kwa meli ikiwemo tukio la Jumapili lilosababisha kutoweka kwa wahamiaji 80 baada ya boti walimokuwa, kuzama wakitokea Libya.
 

Tangu tarehe 28 March watu wasiopunguwa 181 walifariki au hawajulikani waliko kufuatia matukio matano tofauti ya meli kuzama.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet