Kibarua cha kocha Rob Edwards chaota mbawa
Eric Buyanza
June 11, 2026
Share :

Klabu ya Wolverhampton Wanderers imemfuta kazi kocha mkuu Rob Edwards baada ya klabu hiyo kushuka daraja kutoka Ligi kuu ya Uingreza.
Kwa mujibu wa Sky Sports, Edwards alichukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo ya Molineux mwezi Novemba mwaka jana, akichukua nafasi ya Vitor Pereira, lakini Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 43 hakuweza kuizuia klabu hiyo kushuka.
Kocha wa Gil Vicente Cesar Peixoto, ambaye aliiongoza klabu hiyo kumaliza vyema katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu ya Ureno msimu uliopita, atachukua nafasi ya Edwards katika klabu hiyo.





