pmbet

Kiboko ya wezi wa pikipiki anayetikisa Mexico

Eric Buyanza

June 29, 2026
Share :

El Batman de Lagos de Moreno ni jina la utani alilopewa mtu asiyejulikana nchini Mexico, ambaye amekuwa akiwasaka na kuwakamata wezi wa pikipiki.
 

Kazi hii ya kutukuka huwa anaifanya katika mji wa Lagos de Moreno, na imevuta hisia na mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari tangu katikati ya mwezi huu wa Juni 2026.
 

"Batman" huwakamata washukiwa wa wizi wa pikipiki nyakati za usiku na badala ya kuwapeleka polisi anawafunga kwenye nguzo za umeme barabarani ili waonekane na kila mtu nyakati za asubuhi.
 

Baadhi ya washukiwa wamekutwa wakiwa wamechorwa masharubu kwenye nyuso zao, na wengine wameandikwa neno "Rata" kwenye mapaji ya nyuso zao (neno linalomaanisha panya au mwizi kwa Kihispania).
 

Jamaa huyo huacha pikipiki inayodhaniwa kuwa ya wizi pamoja na ujumbe wa maandishi unaowaonya wezi wengine kuwa watafikwa na hali hiyo wakiendelea kuiba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet