Kibwana na Mzize kila mmoja faini milioni 1, kisa kutoa taulo golini
Eric Buyanza
February 16, 2024
Share :
Faini ya shilingi milioni moja kwa Kibwana Shomari inatokana na beki huyo wa kulia wa Klabu ya Yanga, kuonekana akiingia uwanjani na kutoa taulo golini kwa Mashujaa kwenye mechi ambayo Yanga ilishinda mabao 2-1.
Kwa upande wa mshambuliaji wa Klabu hiyo Clement Mzize yeye alionekana akitoa taulo golini kwenye mchezo wao na Dodoma Jiji kwenye mechi ambayo Yanga ilishinda bao 1-0, ambapo na yeye kwa kosa hilo atalipa faini shilingi Milioni moja.