pmbet

Kidume cha mbegu Neymar atarajia mtoto wa tatu!

Eric Buyanza

January 6, 2024
Share :

MBrazil Neymar anatarajia kuwa baba kwa mara nyingine tena, safari hii ikiwa ni mtoto wa tatu.

 

Tovuti ya LeoDias nchini Brazil, imefichua kwamba mama wa mtoto huyo anayetarajiwa ni mwanamitindo ambaye sasa ana ujauzito wa miezi mitatu.

 

Habari za ujauzito huo zilimshangaza pia Neymar mwenye kwa kuwa inaelezwa hakutarajia.

 

Mchezaji huyo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

 

Ni miezi miwili pekee imepita tangu aliyekuwa mchumba wa Neymar, Bruna Biancardi, athibitishe kutengana rasmi na mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG).

 

Bruna aliamua kuachana na Neymar baada ya kufichuka kwa taarifa kuwa staa huyo wa klabu ya Al Hilal ya nchini Saudi Arabia, alimuomba kahaba mmoja wa mtandaoni amtumie picha za uchi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet