pmbet

Kiemba amaliza utata penalti ya Simba kwa Kagera

Sisti Herman

December 16, 2023
Share :

Mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga na timu ya Taifa Tanzania Amri Kiemba ambaye kwasasa ni mchambuzi wa mpira wa miguu amemaliza utata ulioibuka mtandaoni kuhusiana na utata wa bao la pili la kati ya matatu Simba dhidi ya Kagera Sugar lililotokana na mkwaju wa penalti uliopigwa na Saido Ntibanzokiza.

 

“Penati inaweza kurudiwa ikiwa kipa atatoka kwenye mstari kwa sababu alifaidika na makosa yake,lakini pia inaweza kurudiwa ikiwa wachezaji wanaohusika kuzuia watawahi kuingia kwenye 18, hayo yote yataangaliwa ikiwa itakoswa” alisema Kiemba akifafanua sababu za penalti ya Simba kurudiwa mara mbii.

“Lakini pia penati inaweza kurudiwa ikiwa timu inayohusika kufunga wataingia kwenye 18 kabla ya mpigaji kupiga , kwanini mmeingia na mmefunga? kwa hiyo itarudiwa” aliongeza Kiemba kwenye ufafanuzi wake.


“Tukio la leo watu wametazama kama kosa la golikipa kwa sababu aliyeitisha hilo tukio (kibendera) anahusika moja kwa moja kuangalia kama kipa atatoka kwenye mstari, Lakini ukiangalia wachezaji wa timu zote mbili waliingia na mkiingia wote nyie mnaozuia ndio mtaadhibiwa” alihitimisha mchezaji huyo ambaye anatajwa kama mmoja wa wachambuzi mwenye uelewa mkubwa sana wa soka kwasasa nchini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet