Kigogo apigwa kisu kwenye mkutano na wanahabari Korea
Sisti Herman
January 2, 2024
Share :
Kiongozi wa upinzani nchini Korea Kusini, Lee Jae-myung (59) amechomwa kisu shingoni katika mkutano na waandishi wa habari mjini Busan wakati mshambuliaji alipomkaribia kuomba saini yake.
Lee ambaye alikosa urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, anatarajiwa kugombea tena katika uchaguzi ujao unaotarajia kufanyika Aprili 2024.