Kigogo Yanga kuchukua fomu ya Ubunge leo ZNZ
Eric Buyanza
June 28, 2025
Share :
Siku tatu baada ya kuisaidia Yanga SC kuwafunga watani zao Simba SC na kuibuka na Ubingwa wa NBC Premium League, Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga SC @arafat_ah leo anatarajiwa kuchukua Fomu kwa ajili ya kugombea Ubunge, Zanzibar.
Arafat ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya PBZ Visiwani Zanzibar anachukua fomu hiyo ya kuliwania Jimbo la Shaurimoyo visiwani humo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akithibitisha jana kwa kuzungumza na moja ya kituo cha Online Media, Arafat amethibitisha kuwa leo atachukua fomu hiyo kwa ajili kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo hilo.