pmbet

Kihimbwa asimamishwa Fountain kisa kumpiga refa

Sisti Herman

June 13, 2025
Share :

 

Uongozi wa timu ya Fountain Gate FC yenye makazi yake Babati mkoani Manyara imemsimamisha nyota wao Salum Kihimbwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.

Kihimbwa msimu huu amekuwa na kiwango bora katika Ligi Kuu Bara, ambapo amehusika katika mabao tisa ndani ya timu hiyo, akifunga nne na kutoa pasi za mabao matano.

Amesimamishwa kwa muda usiojulikana baada ya kumpiga mwamuzi katika mchezo wa kirafiki ambao Fountain Gate ilicheza dhidi ya Wapolo FC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.

Katika mchezo huo wa kirafiki Kihimbwa alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Wapolo FC ambapo mchezaji huyo alionekana kupinga maamuzi ya mwamuzi wa kati na kumpiga ngumi ya uso. Wakati huo Fountain Gate ilikuwa inaongoza kwa magoli 2-1.

Mratibu wa Fountain Gate FC, Wendo Makau ameiambia Mwanaspoti kuwa wamefikia uamuzi wa kumsimamisha mchezo huyo kwa muda usiojulikana ili kulinda taswira ya timu yao ambayo wameijenga muda mrefu.

"Kwetu sisi kama Fountain Gate mchezaji asipokuwa na nidhamu hata awe na kiwango kizuri vipi tunamtoa kwa hiyo Kihimbwa anaweza kurudi au asirudi," amesema Makau.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wachezaji wote kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ili kulinda taswira ya timu huku wakitambua kuwa mpira ni ajira na ajira yoyote ile inahitaji nidhamu ya hali ya juu.

Fountain Gate FC imeweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi kuelekea mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambazo zimesalia kwa upande wao dhidi ya Coastal Union FC na Azam FC ambazo ni muhimu kushinda ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kukwepa kucheza hatua ya mtoano (play off).
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet