Kihongosi ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Yahaya atumbuliwa
Sisti Herman
June 11, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya uteuzi, Bw. Kihongosi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Bw. Kihongosi anachukua nafasi ya Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.