Kijana acheza na nyuki, asema wadudu hao wanamuelewa
Eric Buyanza
December 23, 2023
Share :
Kijana Tamirat Getachew wa nchini Ethiopia mwenye umri wa miaka 18 amewashangaza wengi kwenye eneo analotoka kwa uwezo wake mkubwa wa kunong'ona na nyuki huku akicheza nao na wala nyuki hao wasimfanye lolote.
Tamirat anawaruhusu nyuki hao kukukusanyika kifuani na kichwani mwake bila kuvaa ulinzi wa aina yoyote. Wakati mwingine hata anaruhusu nyuki kuingia kinywani mwake.
“Nina uwezo maalum wa kujiweka karibu na nyuki bila kuziba midomo na masikio yangu,” anasema.
Inaelezwa kuwa hali hii ya kutokuogopa nyuki ilimuanza miaka 5 iliyopita ambapo Bw Tamirat alianza kuwa karibu na nyuki kwa mara ya kwanza.
Akielezea hali hiyo ilivyoanza Tamirat anasema……“Waliruka na kutulia mwilini wwangu nilipokuwa nikipita karibu na shamba la nyuki, mara nikaona wanaanza kuwa makini na nilichokuwa nikisema,” anamalizia.