Kijana adaiwa kubaka kuku hadi akafa
Eric Buyanza
April 14, 2024
Share :
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Sunday, mkazi wa Kitongoji cha Misungwi Kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza, anadaiwa kubaka kuku hadi kufa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa alimkamata kuku huyo ambaye alikuwa anataga kisha kumuingiza ndani ya nyumba yake na kuanza kumbaka na baada ya kumaliza haja zake akatoka kumtupa nje.
Mmoja wa wapangaji katika nyumba hiyo, Delifina Boazi amesema alitoka nje kwenda kukinga maji bombani ndipo alipomuona mtuhumiwa akifanya kitendo hicho sebleni akiwa amekaa kwenye makochi.
"Nilimuoma alikuwa amemkamata kuku na anafanya naye mapenzi na alipomaliza alienda kumtupa," amesema Delifina.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kitongoji cha Misungwi, Samson Madirisha amekiri kupokea taarifa hizo na baada ya kufika eneo la tukio alikuta kitendo hicho kimeshafanyika.
Madirisha amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa alikuwa na hamu hivyo alishindwa kujizuia.
Baada ya tukio hilo kijana Sunday alichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano.
NIPASHE