Kijana usithubutu kukata tamaa na maisha
Eric Buyanza
April 16, 2024
Share :
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Victor Boniface ametupia picha yake ya enzi hizo akijitafuta....ili kuwahamasisha vijana kutokata tamaa na maisha.
Victor juzi usiku yeye na klabu yake walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ilipoanzishwa miaka 120 iliyopita.
Mchezaji huyu amekuwa na mchango mkubwa sana katika kuiwezesha klabu yake kutwaa ubingwa huo.