Kijana wa miaka 20 ndiye aliyetaka kumuua Trump
Sisti Herman
July 14, 2024
Share :
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) limesema tukio la ufyatuaji risasi iliyomjeruhi Rais wa zamani wa Nchi hiyo, Donald Trump lilikuwa ni jaribio la mauaji na kwamba aliyefyatua risasi alipanga kumuua Trump .
FBI wamesema Kijana mwenye umri wa miaka 20, Thomas Mattew Crooks kutoka Bethel Park, Pennsylvania Nchini Marekani ndiye aliyehusika kurusha risasi hizo ambazo pamoja na madhara mengine risasi moja imemjeruhi Trump kwenye eneo lake la juu la sikio ambapo na yeye pia alipigwa risasi na kuuawa papohapo na Mamlaka za Kiusalama.
FBI imesema bado haijajulikana sababu za Crooks kutaka kumuua Trump na uchunguzi unaendelea “Crooks hakuwa na kitambulisho cha kumtambua kinachoendelea sasa tutahitaji kupima DNA na kuangalia picha zake ili tuweze kupata taarifa zaidi, yoyote mwenye taarifa ambazo zitasaidia uchunguzi anaombwa kutupatia ili zitusaidie”