Kijiji chapasua simu zote za 'Smartphone' kuepuka matapeli
Eric Buyanza
July 2, 2026
Share :

Kijiji cha Sukhpuri huko nchini India kimetikisa vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii kufuatia uamuzi wao wa kuvunja hadharani simu zao za kisasa yaani (Smartphones).
Uamuzi huo ulitolewa na baraza la wazee wa kimila ili kuepuka Uhalifu wa kimtandao kwani eneo hilo limekuwa likisifika kwa ongezeko la makundi ya vijana wanaojihusisha na utapeli na uhalifu wa mitandaoni kwa kutumia simu za 'Smartphones'.
Wanakijiji waliona kuwa matumizi ya kupitiliza ya simu hizo yameharibu mahusiano ya kifamilia, uzalishaji wa kazi, na kuwatazama vijana wakipoteza muda mwingi kwenye simu badala ya kusoma.
Hatua ya kuvunja simu hizo za gharama kubwa ilikuwa ishara ya kiapo cha vijana hao kuacha uhalifu, kufanya kazi kwa juhudi, na kuishi kwa kufuata sheria.
Baada ya zoezi hilo la kuharibu simu, uongozi wa kijiji uliamua kuwa wanakijiji wote waanze kutumia simu za 'vitochi' au kwa jina lingine 'Viswaswadu' jambo litakalosaidia kupunguza ushawishi wa mitandao na kulinda maadili ya jamii hiyo.





