pmbet

Kiki ya Malkia Karen yamuharibia kwa mashabiki.

Joyce Shedrack

April 21, 2026
Share :

Mashabiki wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Malkia Karen wamekerwa na kitendo cha msanii huyo kutengeneza kiki ya kupigwa aliyoitengeza siku ya jana kwa ajili ya kuachi filamu yake ya ‘guilt of love’.

Hali hii inakuja mara baada ya chapisho la siku ya jana Aprili 20, kutoka kwa Karen ambalo kwa sasa limeshafutwa lililoonyesha picha zinazoashiria kupigwa na mwanaume aliyedai kuwa ni mzazi mwenzake.

Sambamba na picha hizo chapisho hilo liliambatana na ujumbe uliosema: "Imagine Mwanaume anampiga Mwanamke Namna hii Kisa Mapenzi? Tena mwanamke asiyejua ugomvi wala kupigana? Na nimepigwa usiku nikiwa helpless, sina nguvu wala hakukua na mtu mwingine yoyote wakunitetea. Hivi ndivyo baba watoto wangu ameamua kunifanyia. Naumwa Kichwa mwili mzima, nimegongwa zaidi ya mara sita ukutani..."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet