KIKOSI CHA CHUMA: Mourinho ataja wachezaji 4 ambao nafasi zao hazigusiki
Eric Buyanza
August 19, 2026
Share :

Kwa mujibu wa gazeti la michezo la AS la Uhispania, Kocha mpya wa Real Madrid, Jose Mourinho, amebainisha wachezaji wanne wa safu ya ushambuliaji ambao nafasi zao hazitagusika msimu huu.
Wachezaji hao wanne wa mbele ambao wametajwa kuwa nguzo kuu ya mfumo wake wa 4-2-3-1 ni:
Kylian Mbappé, Vinícius Júnior, Jude Bellingham na Yan Diomandé.
Mbali na wachezaji hao wanne wa mbele, kipa Thibaut Courtois naye ametajwa kama mchezaji mwingine asiyejadilika katika kikosi chake cha kwanza.
Mourinho anapanga kuwatumia mastaa hawa kuunda safu hatari ya ushambuliaji kuelekea ufunguzi wa msimu wa LaLiga dhidi ya Espanyol siku ya Jumamosi.





