pmbet

Kikosi cha mwisho cha Serengeti Boys kuelekea AFCON U17

Sisti Herman

May 6, 2026
Share :

 

Baada ya jana Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya Umri wa miaka 17 'Serengeti Boys' kushinda 3-1 kwenye mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Cameroon katika uwanja wa Mohammed V Casablanca, Morocco kwaajili ya maandalizi ya mwisho ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON U17), kocha mkuu wa timu hiyo Elieneza Nsanganzelu ametaja kikosi rasmi cha timu hiyo kitakachocheza mischuano hiyo.

Timu ya Serengeti Boys ipo nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Vijana za AFCON 2026 zinazofanyika chini Morocco 🇲🇦 Fainali hizo zitaanza Mei 13,2026 mpaka June 2, 2026.

Timu ya Vijana ya Tanzania imepangwa kundi C pamoja na nchi za Mozambique, Angola na Mali.

Timu nane zitakazofuzu kucheza hatua ya Robo Fainali na Best Loosers wawili zitakuwa zimefanikiwa kucheza Fainali za U17 Kombe la Dunia 2026 nchini Qatar.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet