Kila nikienda Afrika siwezi kutembea kuna 'Machizi soka' kila mahali
Eric Buyanza
February 20, 2024
Share :
Kocha wa kireno mwenye vituko Jose Mourinho amesema ana washkaji wengi Afrika wanaompenda huku akiwataja baadhi yao kuwa Didier Drogba, John Obi Mikel na Michael Essien.
Akizungumza kwenye mahojiano na podcast ya gwiji la Manchester United, Rio Ferdinand, Mourinho aliwasifu wachezaji wa kiafrika na kusema ni waaminifu sana.
Akizungumzia swala la kuja Afrika, kocha huyo anasema....."Siwezi kwenda Afrika kwasasa. Kuna 'machizi soka' kila mahali....kila nikienda Afrika siwezi kutembea...vijana wananipenda. Hata ulaya yenye vijana wengi wa kiafrika watu wananipenda sana."