pmbet

Kilio cha wana-Simba kuhusu Kayoko chasikika, aweza kuadhibiwa!

Eric Buyanza

February 15, 2024
Share :

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni, amewaambia wanachama na mashabiki wa Simba kuwa wamesikia kilio chao dhidi ya mwamuzi Ramadhani Kayoko na jambo hilo litakwenda kufanyiwa kazi na Kamati na Nidhamu na anaweza kuadhibiwa iwapo itathibitika kuwa alikuwa na mapungufu kwenye uamuzi wake.
 

Ijumaa iliyopita baada ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Azam FC kumalizika, mashabiki wa 'Wekundu wa Msimbazi' hao walifanya maandamano ndani ya uwanja wa CCM Kirumba, wakimshutumu mwamuzi huyo kwa kutochezesha mechi hiyo kwa haki, wakidai aliwanyima haki kwenye baadhi ya matukio na kuwafanya kutoka sare ya bao 1-1.
 

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Hamduni aliwaomba radhi mashabiki na wadau wote waliokwazwa kwa njia moja ama nyingine kutokana na ufanyaji kazi wa waamuzi katika mechi za hivi karibuni ambazo zimeonekana kuwa na malalamiko mengi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet