Kim atoa heshima kwa wanajeshi wake waliouawa Ukraine
Eric Buyanza
July 1, 2025
Share :
Vyombo vya habari vya serikali Korea Kaskazini vimemuonesha Kim Jong Un akitoa heshma za mwisho mbele ya majeneza ya wanajeshi wa taifa lake yaliovishwa bendera, ambao waliuawa wakiisaidia Urusi kukabiliana na Ukraine.
Duru kutoka Korea Kusini zimesema hakujawa na dalili za kupelekwa kwa wanajeshi zaidi nchini Urusi katika vita hivyo. Korea Kaskazini yenye kujihami kwa silaha za nyuklia imekuwa mojawapo ya washirika wakuu wa Urusi wakati wa mashambulizi yake ya zaidi ya miaka mitatu kwa Ukraine, na kutuma maelfu ya wanajeshi na shehena ya silaha kuisaidia Kremlin kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine kutoka katika eneo la Kursk.
Takriban wanajeshi 600 wa Korea Kaskazini wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa wakipigania Urusi, kwa mujibu wa mbunge wa Korea Kusini Lee Seong-kweun, akinukuu taarifa kutoka kwa shirika la kijasusi la Seoul.