Kim Jong Un kutuma wanajeshi 30,000 zaidi kuisaidia Urusi vita
Eric Buyanza
July 3, 2025
Share :
Korea Kaskazini inakusudia kuongeza mara tatu idadi ya wanajeshi wake wanaopigana upande wa Urusi katika vita na Ukraine, na kutuma wanajeshi wa ziada 25,000 hadi 30,000 kusaidia Moscow, kulingana na shirika la ujasusi la Ukraine.
Shirika la habari la Marekani CNN limeinukuu taarifa ya ujasusi ya Ukraine ikisema, Wanajeshi hao wanaweza kuwasili Urusi katika miezi ijayo, na kuongeza kuwa jumla ya wanajeshi 11,000 wa Marekani walilpelekwa Urusi Novemba mwaka jana kujibu uvamizi wa Ukraine katika eneo la Kursk.
CNN ilikagua picha za satelaiti na kuona kwamba meli ya Urusi ya Ropucha, ambayo wachambuzi wanakadiria kuwa inaweza kubeba hadi wanajeshi 400 na ilitumika mwaka jana kupeleka wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi, ilitia nanga tena kwenye bandari ya Danube karibu na Nakhodka mnamo Mei.
Ndege za mizigo pia zilionekana katika Uwanja wa Ndege wa Sunan huko Korea Kaskazini.
Inaaminiwa kuwa hizi zinaweza kuwa ishara za kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Ukraine siku zijazo.
BBC