Kim Kardashian afunguka Kanye West kugawa magari yao ya kifahari kwa marafiki zake.
Joyce Shedrack
October 16, 2025
Share :
Staa na Mfanyabiashara maarufu wa Marekani Kim Kardashian amefunguka kuhusu aliyekuwa mume wake Rapa Kanye West akiweka wazi kuwa aliwahi kugawa magari yao ya kifahari aina ya Lamborghini kwa marafiki zake.

Kupitia mahujiano aliyofanya na 'Call her Daddy' hivi karibuni Kim amesema aliwahi kurudi nyumbani na kukuta Lamborghini zao tano hazipo na alipomuuliza mumewe akasema aliwapa marafiki zake.
"Nilirudi nyumbani tulikuwa na Lamborghini tano, nilikuta zote hazipo nikamuuliza zipo wapi gari zetu mpaka gari yangu mpya, aliwapa marafiki zake gari zote" Amesema Kim Kardashian.
Kingine ambacho amefunguka Kim ni ugumu anaopitia kwa Kanye West katika kushirikiana malezi ya watoto wao wanne baada ya ndoa yao kuvunjika rasmi mwaka 2022.