Kim Kardashian ashutumiwa kumuiga mke wa Kanye, apewa jina 'Kim Censori'
Eric Buyanza
March 27, 2024
Share :
Aliyekuwa mke wa zamani wa Kanye West, Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Kim Kardashian ameshutumiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameanza kumuiga kimavazi mke wa sasa wa Kanye West, mwanamitindo Bianca Censori.
Mwanadada Bianca mwenye asili ya Australia, anafahamika kwa uvaaji wake wa mavazi ambayo mara nyingi huacha wazi baadhi ya sehemu za maungo yake kiasi cha kuwakera hata wazazi wake.
Kim Kardashian jana tarehe 26 March kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha akiwa amevalia kivazi ambacho kiliacha wazi sehemu ya maziwa yake.
Baada ya picha hiyo ndipo raia walipomwagika kila kona ya mitandao ya kijamii wakimpachika jina 'Kim Censori'...wengi wao wakisema anamuiga Bianca na wengine kwenda mbali zaidi na kudai anafanya hivyo siku chache baada ya kutengana mpenzi wake Odell Beckham Jr (OBJ).
Hata hivyo wapo pia waliomtetea Kim, wakisema hilo ni vazi kama mavazi mengine na Bianca sio wa kwanza kuvaa mikato ya namna hiyo.
Jumapili ya tarehe 24 gazeti la Daily Mail lilikuwa la kwanza kuchapisha habari ya kutengana kwa Odell Beckham Jr na Kim Kardashian.