Kim na Khole walivyotupia mavazi ya kihindi kwenye harusi ya mtoto wa Bilionea wa India
Sisti Herman
July 14, 2024
Share :
Hivi ndivyo ndugu wawili Kim na mdogo wake Khloe Kardashian walivyopigilia mavazi jana katika siku ya pili ya harusi ya mtoto wa bilionea, Anant Ambani na mkewe Radhika Merchant ambao ndoa yao ilifungwa Ijumaa.
Ndugu hao ambao wamekuwa wakitikisa kwenye masuala ya urembo siku ya pili walitupia mavazi ya Kihindi huku Kim akiwa na vito vilivyozunguka kutoka kwenye pua ya kushoto na sikio la kushoto na Khloe akiwa amevalia vito masikioni na shingoni, jambo lililopelekea wadau mbalimbali wa mitindo kudai wawili hao walijipanga zaidi kwa sherehe hiyo.