Kimenuka Kongo, M23 yaushikilia mji mwinine
Eric Buyanza
March 8, 2024
Share :
Waasi wa M23 wamedhibiti eneo jingine, wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya tatu mashariki mwa Kongo. Maelfu ya raia wanaendelea kuyakimbia makaazi yao wakitafuta usalama sehemu nyingine.
Waasi wa M23 wamedhibiti eneo jingine, wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya tatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Maelfu ya raia wanaendelea kuyakimbia makaazi yao wakitafuta usalama.
Duru zinasema kufikia jana, M23 walikuwa wameudhibiti mji wa Kibirizi, kilometa 30 upande wa Kaskazini Mashariki.
Afisa mmoja wa utawala katika eneo hilo alilieleza shirika la habari la AFP kwamba, M23 walidhibiti mji huo baada ya kufyatuliana risasi na wanajeshi wa serikali ya Kongo na wapiganaji wanaoiunga mkono serikali.