Kinda aliyewaua Liver ajitoa mitandaoni kisa Ramadhan
Sisti Herman
March 19, 2024
Share :
Kinda wa Manchester United Amad Diallo ambaye aliwaka sana kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Liverpool wiki iliyopita amefuta akaunti zake zote za mitando ya kijamii kwasababu ya mwezi mtukufu wa Ramdhan.
“Nimefuta akaunti zangu za mitandao ya kijamii zote ili nizingatie zaidi Ramadhan kwasababu kwenye mitandao naweza kuona vitu vibaya ambavyo vinaweza kuathiri mfungo wangu” Diallo alibainisha kupitia jarida la ESPN.
Diallo aliibuka nyota wa mchezo baada ya kuisaidia United kufuzu robo fainali ya kombe la FA baada ya kufunga bao la ushindi dakika za nyongeza baada ya zile 120 za mchezo huo uliomalizika kwa Man Utd kushinda mabao 4-3.