pmbet

Kinda Madrid atwaa taji la 5 Brazil akiwa na miaka 17 tu

Sisti Herman

April 8, 2024
Share :

Mara baada ya jana klabu yake ya sasa ya Palmerias kutwaa taji la Paulista dhidi ya Santos huko Brazil, kinda ajaye wa Real Madrid Enfrick sasa ameweka rekodi ya kutwaa makombe matano makubwa nchini humo akiwa na miaka 17 tu kabla kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.

 

Kinda huyo amekuwa na mfululizo bora kwenye wiki tatu zilizopita kwani alifunga bao lake la kwanza akiwa kwenye dimba la Wembey akiwa na uzi wa Brazil dhidi ya Uingereza kabla ya kuwafunga tena Hispania kwenye dimba la Santiago bernabeu siku 3 baadae.

 

Mara baada ya kumalizika kwa ratiba za timu ya taifa Endrick alirudi kwenye klabu yake ya sasa Palmerias ambapo siku 2 baada alifunga bao la pekee lililowapeleka fainali ambayo wametwaa taji hilo jana.

 

Hadi sasa akiwa na miaka 17 tu, tayari Endrick ameshatwaa makombe matatu akiwa na Plamerias ambayo ni Kombe la ligi kuu Brasileiro mara mbili, Kombe la Paulista mara mbili na Brazil Supercopa.

 

Endrick msimu ujao anajiunga na Real Madrid kutokea Palmerias.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet