pmbet

Kinda wa Madrid aliwafunga England na kuweka rekodi mpya

Sisti Herman

March 24, 2024
Share :

Baada ya kufunga goli la pekee lililowapa ushindi timu ya taifa ya Brazil mbele ya Uingereza kwenye dimba la Wembley, kinda mpya wa Real Madrid Endrick sasa anakuwa mchezaji kinda zaidi kuwahi kufunga goli kwenye dimba hilo kubwa zaidi England na la pili barani Ulaya.

Endrick mzaliwa wa mwaka 2006 baada ya kombe la dunia, amefunga goli hilo dakika 9 baada ya kutoka benchi dakika ya 71 akichukua nafasi ya Rodrigo.

Pia Endrick anakuwa mchezaji kinda zaidi kuwahi kufunga goli kwenye timu ya Taifa baada ya Ronaldo De Lima aliyefanya hivyo mwaka 1994.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet