Kinda wa Madrid avunja rekodi ya Rolnado kwenye Euro.
Joyce Shedrack
June 19, 2024
Share :
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uturuki Arda Guler amevunja rekodi ya Cristiano Ronaldo iliyodumu kwa miaka 20 ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Mataifa ya Ulaya EURO 2024 inayoendelea nchini Ujerumani.
Ronaldo alifunga goli dhidi ya Czechia kwenye michuano ya EURO 2004 iliyofanyika nyumbani kwao Ureno akiwa na umri wa miaka 19 na siku 128
Siku ya jana Arda Guler alifunga goli kwenye michuano ya EURO 2024 timu yake iliposhuka katika dimba la Signa Iduna Park kumenyana na Georgia na kuibuka na ushindi wa goli 3-1 akiwa na umri wa miaka 19 na siku 114.