pmbet

Kinda wa Nigeria ahukumiwa jela miezi 6 kwa unyanyasaji wa kingono.

Joyce Shedrack

March 12, 2026
Share :

Mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Nchini Nigeria Daniel Daga amekutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela kufuatia tukio lililomhusisha mwanamke mwaka mmoja uliopita.

 

Hukumu hiyo ilitangazwa Jumanne na Mahakama ya Wilaya nchini Norway ambapo mbali na kifungo hicho cha jela, mahakama pia iliamuru Daga kulipa gharama za kisheria kama ilivyoombwa na upande wa mashtaka.

Nigeria U20 player Daniel Daga jailed in Norway for sexual assault |  TheCable

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye anacheza katika klabu ya Molde FK, alikabiliwa na tuhuma za kumshambulia kingono mwanamke ambaye hakutajwa jina tukio hilo linalodaiwa kutokea mwezi Aprili, huku mashtaka yakifunguliwa tarehe 19 Desemba 2025.

 

Licha ya kutiwa hatiani, wakili wake, Astrid Bolstad, ameendelea kusisitiza kuwa mteja wake hana hatia. Alidai kuwa tukio hilo lilikuwa la makubaliano kati ya pande zote na akatangaza kuwa wata kata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.

 

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, klabu ya Molde FK ilitoa taarifa ikithibitisha kuwa Daga amesimamishwa kucheza kwa muda usiojulikana “Kutokana na hali ilivyo na mchakato wa kisheria unaoendelea, klabu imeamua kuwa mchezaji huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha mechi hadi itakapotangazwa vinginevyo,” klabu hiyo ilisema.

 

Daga, ambaye anacheza nafasi ya kiungo katika timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya miaka 20 alijiunga na Molde FK mwanzoni mwa msimu wa 2025 na tangu wakati huo amecheza mechi 15, akifunga mabao matatu kwa klabu hiyo ya Norway.

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet