pmbet

Kinda wa Tanzania, Hasnath ajiunga na TUT FC ya Misri

Sisti Herman

July 30, 2024
Share :

Kampuni ya usimamizi wa wachezaji ya Kitanzania Jeff Sports Management imethibitisha rasmi kuwa kiungo mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Tanzania Hasnath Linus Ubamba amejiunga na klabu ya Tutankhamum FC ya ligi kuu wanawake nchini Misri akitokea Fountain Gate Princess ya ligi kuu wanawake Tanzania.

Hasnath anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Fountain Gate Princess kujiunga na timu hiyo ya ligi kuu Misri baada ya mshambuliaji wa timu ya Taifa Burundi Niyonkuru Sandrine na Kiungo wa timu ya Taifa Tanzania Suzan Adam.

Hasnath amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet