KInda watano wa Man U wajumuishwa kikosi cha wakubwa.
Joyce Shedrack
February 5, 2026
Share :
Manchester United ilikuwa na vijana wake watano akiwemo mshambuliaji JJ Gabriel walioshiriki mazoezini kabla ya pambano lao na Tottenham Jumamosi.
Chini ya Michael Carrick aliyepewa timu kwa muda hadi sasa ameshinda mechi 3 za ligi, na anataka ushindi wa nne Jumamosi hii.
Jack Moorhouse alikuwa mmoja wa vijana kadhaa walioshiriki mazoezi Jumatano. Hivi majuzi amerejea kutoka kwa mkopo Leyton Orient na anatafuta kuendelea baada ya hivi karibuni kurudi Manchester.
Jack na Tyler Fletcher pia walionekana wakifanya mazoezi mbele ya kamera za MUTV.
Wao ni watoto wa mchezaji wa zamani Darren Fletcher ambaye bado yuko katika kikosi cha klabu hiyo na alikuwa kocha wa muda wa timu hiyo kwa michezo miwili kabla ya kuteuliwa kwa Carrick hadi mwisho wa msimu.
Beki wa pembeni Yuel Helafu, mwenye umri wa miaka 17, pia alikuwa mazoezini.
Mshambuliaji Gabriel, mwenye umri wa miaka 15, pia alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza wakati wa mazoezi. Hastahili kucheza katika michezo ya Ligi Kuu, lakini ana kiwango cha juu katika klabu hiyo na amefunga mabao 11 katika michezo 16 kwa akademi msimu huu huku wengi wakimpigia debe kwa mambo makubwa.





