Kindoki atambulishwa Yanga
Sisti Herman
January 17, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imemtambulisha shabiki maarufu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari wa timu hiyo Jimmy Kindoki kuwa afisa wa idara ya wanachama wa klabu.
Idara hiyo kabla ilikuwa chini ya CPA. Haji Mfikirwa ambaye mkataba wake kuitumikia timu hiyo ulitamatika mwishoni mwa mwaka jana.