'King Kazu', atacheza msimu ujao akiwa na umri wa miaka 58
Eric Buyanza
November 27, 2024
Share :
Kazuyoshi Miura, ambaye mara nyingi hujulikana kama 'King Kazu', ni mchezaji wa soka wa Kijapani anayekipiga kama mshambuliaji wa klabu ya Atletico Suzuka, inayoshiriki Ligi ya Soka daraja la nne.
Miura ana umri mkubwa mno ukilinganisha na wachezaji wenzake ambao wengine kwa umri ni kama watoto wake.
Ni jambo la kushangaza lakini ukweli ni kwamba watu wa umri wake walistaafu soka miaka 30 iliyopita.
Miura atafikisha umri wa miaka 58 mwezi Februari 2025, lakini bado ana nia ya kuendelea kucheza msimu ujao.
Kama atafanikiwa kucheza msimu ujao kama anavyotaka, basi utakuwa msimu wake wa 40 kwenye soka la kulipwa.