Kinondoni yaongoza kwa makosa ya jinai Tanzania 2025
Sisti Herman
October 27, 2026
Share :

Taarifa ya hivi karibuni ya Jeshi la Polisi Tanzania imeitaja Kinondoni kuwa eneo lililorekodi idadi kubwa zaidi ya makosa makubwa na madogo ya jinai nchini mwaka 2025.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, makosa makubwa 46,334 na makosa madogo 549,215 yalirekodiwa nchini kote, hali inayochochea wito wa kuimarishwa kwa mikakati ya kuzuia uhalifu.
**Maeneo yaliyoongoza kwa makosa makubwa ya jinai:**
1. Kinondoni — 3,407
2. Mara — 2,820
3. Tanga — 2,508
4. Kilimanjaro — 2,480
5. Pwani — 2,208
**Maeneo yaliyoongoza kwa makosa madogo ya jinai:**
1. Kinondoni — 64,814
2. Mwanza — 47,781
3. Temeke — 37,590
4. Ilala — 34,199
5. Morogoro — 29,917
Wataalamu wanasisitiza kuwa kupambana na uhalifu kunahitaji zaidi ya hatua za kisheria. Wanashauri kuongeza fursa za ajira, mikopo nafuu, mafunzo ya ufundi na uwezeshaji wa vijana kujiajiri.
Pia, wanapendekeza kuimarisha ulinzi shirikishi, ushiriki wa wananchi katika kuzuia uhalifu, kuwawezesha waliomaliza vifungo kurejea katika jamii na kupanua huduma za afya ya akili, ushauri nasaha na udhibit





