pmbet

Kiongozi mkuu wa hamas ismail haniyeh ameuawa

Eric Buyanza

July 31, 2024
Share :

Kiongozi mkuu wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh ameuawa mjini Teheran leo Jumatano, kulingana na taarifa zilizotolewa na Hamas pamoja na na kikosi cha ulinzi cha Iran.

Hakuna mpaka sasa aliyekiri kuhusika na mauaji hayo, lakini hapo awali Israel iliwahi kuahidi kuwa itamuua Haniyeh na viongozi wengine wa Hamas baada ya shambulio la kigaidi la Oktoba 7 ndani ya Israel.

Katika taarifa yake, Hamas ilisema Haniyeh, aliuawa kikatili kwenye makazi yake mjini Teheran.

Siku ya Jumanne Haniyeh alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Iran Massoud Pezekshian.

“Mapema asubuhi hii, makazi ya Ismail Haniyeh mjini Teheran yalishambuliwa, yeye na mmoja wa walinzi wake waliuawa. Sababu ya mauaji hayo inachunguzwa na itatangazwa baadaye,” Kikosi cha Revolutionary Guards kimesema.

Televisheni ya serikali ya Iran imeripoti kuhusu kifo cha Haniyeh mapema leo asubuhi.

Israel bado haijajibu au kutoa taarifa yoyote mpaka sasa. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet