Kiongozi mkuu wa Iran aapa kuipa israel 'adhabu kali'
Eric Buyanza
July 31, 2024
Share :
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameapa kutoa kile alichokiita adhabu kali kwa Israeli baada ya mauaji ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran, Israel inatuhumiwa kwa mauaji hayo.
Katika taarifa iliyorushwa na shirika la habari la Iran (IRNA), Khamenei amesema; "Kwa kitendo hiki, utawala wa Kizayuni unaojihusisha na mauaji na ugaidi umejitengenezea adhabu kali, na tunaona kuwa ni wajibu wetu kulipiza kisasi cha damu ya Haniyeh iliyomwagwa katika ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,"
Kundi la Hamas limedai kuwa Haniyeh aliuawa kwenye makazi yake mjini Tehran katika shambulio la anga la Israel baada ya kutoka kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mpya wa Iran.