Kiongozi wa kundi la kipalestina linaloipinga Hamas auawa
Eric Buyanza
December 5, 2025
Share :

Vyombo vya habari nchini Israel vimeripoti kuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina linalopinga Hamas katika Ukanda wa Gaza ameuawa.
Tukio hilo linatazamwa kama pigo kwa juhudi za Israel kuunga mkono makabila ya Kipalestina katika kukabiliana na harakati za Hamas.
Yasir Abu Shabaab, kiongozi wa kabila la Wabedui aliyekuwa akiishi Rafah kusini mwa Gaza, alikuwa akiongoza kundi kuu miongoni mwa makundi madogo yaliyopinga Hamas tangu kuanza kwa vita zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Hamas ilisema kwamba kuuawa kwa Yasser Abu Shabab ni “hatima isiyoepukika kwa wale wote wanaoisaliti nchi na watu wao, na wanaokubali kuwa vyombo vya uvamizi.”





