pmbet

Kiongozi wa serikali akamatwa na mabunda ya fedha nyumbani kwake

Eric Buyanza

June 5, 2026
Share :

Afisa Mkuu wa Mipango ya Miji wa Kaunti ya Nairobi, Patrick Analo Akivaga, amekamatwa na maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kufuatia uchunguzi wa tuhuma za mali isiyoelezeka na utoaji wa vibali vya ujenzi visivyo halali.
 

Katika operesheni iliyofanyika nyumbani kwake Syokimau, maafisa wa EACC walidai kukuta zaidi ya Sh65 milioni taslimu, zikiwemo Sh51.3 milioni na dola za Marekani 113,000, zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye mifuko na ndani ya gari lake.
 

Pia walinasa hati mbalimbali za ardhi na magari, vifaa vya kielektroniki, mikataba ya mauzo pamoja na nyaraka za vibali vya ujenzi vya Kaunti ya Nairobi.

 

Kwa mujibu wa EACC, uchunguzi unaonyesha uwepo wa mali zinazodhaniwa kutolingana na kipato halali cha afisa huyo, huku ukihusishwa na mtandao wa rushwa katika utoaji wa vibali vya majengo yasiyokidhi viwango vya usalama.

 

Analo, ambaye amewahi kushika nafasi za juu katika idara ya Mipango ya Miji na kuwa Kaimu Karani wa Kaunti, amekuwa akitajwa katika tuhuma za utoaji wa vibali vya ujenzi kinyume cha taratibu. Mwaka 2024 alijikuta akichunguzwa na Bunge la Kaunti ya Nairobi baada ya mamia ya miradi ya ujenzi kuibua maswali kuhusu mchakato wa uidhinishaji.
 

Tuhuma hizo zimeibuka wakati Nairobi ikiendelea kukumbwa na matukio ya majengo kuporomoka yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 11. Uchunguzi wa baadhi ya majengo hayo umeonyesha kuwa yalijengwa kinyume na vibali vilivyotolewa awali.
 

Chanzo: Taifa Leo 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet