pmbet

Kiongozi wa Wahouthi atishia waziwazi kushambulia Saudi Arabia

Eric Buyanza

July 17, 2026
Share :

Kiongozi wa kundi la Wahouthi, Abdul Malik al-Houthi, ametishia waziwazi kushambulia viwanda vya mafuta na miundombinu muhimu nchini Saudi Arabia

Kufuatia mapigano na mashambulizi ya anga yaliyoharibu uwanja wa ndege wa Sana'a, kiongozi huyo alitoa hotuba kupitia televisheni akionya kuwa Saudi Arabia itashambuliwa kijeshi ikiwa itajihusisha na mashambulizi dhidi ya maeneo yao nchini Yemen. Alisisitiza msimamo wao kwa kusema: "Mlinganyo wetu ni viwanja vya ndege kwa viwanja vya ndege, bandari kwa bandari, na vikwazo kwa vikwazo.".
 

Hali hii imejitokeza baada ya Wahouthi kuvunja usitishaji wa mapigano uliodumu kwa miaka minne kwa kuvurumisha makombora yaliyolenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abha nchini Saudi Arabia, ingawa makombora hayo yalidhibitiwa na mifumo ya ulinzi ya nchi hiyo. Tishio hili jipya limeibua hofu kubwa ya kurejea kwa vita kamili katika ukanda huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet