Kipa wa Azam FC afariki kwa ajali ya pikipiki.
Joyce Shedrack
September 11, 2026
Share :
Klabu ya Azam FC imetangaza kifo cha kipa wa timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20), Iddy Salim, aliyefariki dunia jana Alhamisi baada ya kupata ajali ya pikipiki.

Azam FC imesema mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala (MRRH), Dar es Salaam, ambako taratibu za awali zinaendelea kabla ya kusafirishwa kwenda Tanga, kwa ajili ya maziko.
Azam FC imetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo, huku ikiwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.





