pmbet

Kipa wa Ronaldo kuchukua nafasi ya Ederson Man City

Sisti Herman

July 21, 2025
Share :

 

Klabu ya Manchester City imefanya mawasiliano ya awali kwa ajili ya kumsajili Diogo Costa, mlinda mlango wa klabu ya FC Porto, na inafikiria kuwasilisha ofa ya takribani €60 milioni.

City inaangalia uwezekano wa kumleta nyota huyo wa Kireno kama sehemu ya mipango yao ya kuimarisha safu ya ulinzi, hasa langoni.

Diogo Costa amekuwa kwenye kiwango bora akiwa na Porto na pia ni chaguo la kwanza kwenye timu ya taifa ya Ureno, jambo linalovutia vilabu vikubwa barani Ulaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet