Kiporo cha JKT na Yanga kupigwa leo
Sisti Herman
April 24, 2024
Share :
Mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya JKT Tanzania na Yanga iliahirishwa kuchezwa siku ya jana baada ya mazingira ya uwanja kuathiriwa na mvua iliyosababisha uwanja kujaa maji imepangwa kuchezwa leo kwenye dimba lilelile la Meja Jen. Isamuhyo majira ya jioni.
Yanga wanaoongoza msimamo wa ligi watachuana na JKT iliyopo nafasi YA 15 kati ya timu 16.