pmbet

Kisa afya Trump atamba kuwa imara kuliko Biden kucheza Golf.

Joyce Shedrack

June 28, 2024
Share :

Rais wa Marekani Joe Biden na Mpinzani wake Donald Trump leo alfajiri wamejibizana kupitia mdahalo wa kwanza wa uchaguzi wa Rais utakaofanyika November mwaka huu.

 

Biden na Trump wametambiana kuhusu rekodi zao mbalimbali za masuala ya kiuchumi huku Trump akitamba uwezo wa sasa kiafya na kimwili kuwa bora kushika dola kuliko Biden akatoa mfano kuwa Biden kutokana na afya yake kudorora kwasababu ya umri mkubwa hawezi kusukuma gofu kwa mita 45.

 

Marais hao wawili wanaingia kwenye rekodi ya kuwa Marais wenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuwania nafasi hiyo Biden akiwa na umri wa miaka 81 na Trump mwenye umri wa miaka 78.

 

Silaha kubwa aliyokuwa akiitumia Biden kwenye mdahalo huo ya kumshambulia Trump ni hatia zinazomkabili Rais huyo wa zamani akisema kama Trump atachaguliwa atakuwa Rais kwanza aliyehukumiwa kwa uhalifu kuingia Ikulu ya Nchi hiyo White House.

 

Trump alijibu mapigo kwa Biden akitilia shaka afya yake na uwezo wake wa kutamka maneno kutokana na Biden wakati mwingine kukisikika akishindwa kukamilisha sentensi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet