pmbet

Kisa Manoo, Eriksen hana furaha Man Utd

Sisti Herman

March 19, 2024
Share :

Mara baada ya kinda Kobbie Mainoo kukiwasha sana siku za karibuni na kuwasugulisha benchi wachezaji wa daraja kubwa ikiwa ni nusu msimu tu tangu apandishwe kwa wakuwa kutokea timu ya vijana, kiungo wa kati wa Manchester United na nahodha wa timu ya Taifa ya Denmark Christian Eriksen amesema wazi kuwa hana furaha kwasasa ndani ya klabu hiyo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

 

"Nimekuwa na mazungumzo na Erik ten Hag kuhusu kutokuwa na furaha hivi sasa ... na kutaka kucheza kadri niwezavyo".

 

"Alisema Kobbie Mainoo anaendelea vizuri na sehemu nyingine ya kiungo pia inafanya vizuri, hivyo kuna ushindani".

 

"Kwa kweli, unaweza kuwa na wasiwasi kwa muda mrefu kwa sababu ninataka kucheza kadri niwezavyo. Hutaki tu kukaa kwenye benchi kila wakati", Eriksen alisema - kupitia jarida la Tipsbladet.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet